Showing posts with label Kazi pendwa. Show all posts
Showing posts with label Kazi pendwa. Show all posts

Sunday, March 25, 2018

NYUMBA YA VYUMBA VITATU VIKUBWA

Hii ni nyumba ya vyumba 3,iliyosanifiwa kwa kuzingatia wale wanaopenda vyumba vikubwa kiasi na wenye eneo la kutosha kujenga na kuifurahia mandhari inayozunguka nyumba

Unaweza kujenga nyumba hii kwenye kiwanja chenye ukubwa kuanzia meta 18 kwa 25.

Mvuto wake na mpangilio  ndani na nje utakufanya ufurahie kuishi na kuiita nyumbani



NYUMBA YA VYUMBA 3

Hii ni nyumba ya vyumba vitatu ambayo inajumuisha sebule,chumba cha chakula(dining), jiko lenye stoo ,common toilet na chumba kimoja kati ya hivyo vitatu ni self contained.
Unaweza kuijenga kwenye kiwanja cha meta 15 kwa meta 20 na kupata nafasi ya kuegesha gari,kucheza watoto,kupumzika na shughuli nyingine muhimu


mwonekano wa upande mmoja,nyuma ya nyumba

mwonekano wa mbele
Je,ni nini imekuvutia kwenye nyumba hii?Niandikie maoni yako,
Wasilisha Email: nyumbaboratz@gmail.com

MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA UNAPOBUNI NA KUJENGA NYUMBA



1.MLANGO MKUBWA WA KUINGIA NDANI(MAIN DOOR)
picha kwa hisani ya Pongu J

Mlango mkuu wa kuingia kwenye nyumba ndio unaokaribisha anayeingia ndani.Kiimani ni lango la kukaribisha nguvu zote zenye faida na zenye madhara.Pia ni mlango mkuu wa kutoka ndani ya nyumba.
·         Ni muhimu mlango wa kuingia ndani uoane ama uwe katika uelekeo mmoja na lango kuu la kuingia (Gate)

·         Lango kuu(gate)  na mlango wa kuingia ndani ni vema view upande mmoja. Sababu kubwa ni kufanya kuwa na urahisi kuingia lango kuu na kutembea moja kwa moja kwenda kwenye mlango wa nyumba pasipo kuzinguka.Pia ni rahisi kujua anayeingia na kutoka
·         Mlango mkuu wa kuingia ni muhimu uwe mkubwa na iwe miwili(double door) yaani ufunguke sehemu mbili.

Pia ni muhimu nyumba kuwa na milango miwili ya nje kuruhusu kuingia na kutoka kwa urahisi pale inapohitajika, na kufanya hewa kuingia na kutoka na kuufanya mzunguko wa hewa ndani ya nyumba

·         Upande wa kuingia unapaswa kuwa mkubwa kuliko wa kutoka.Sababu kubwa ni kwamba,hapa ndipo hewa(air) inavuma kutoka nje kwenda ndani.Unapaswa iignie kwa wingi na kutoka kidogo kufanya nyumba ipumue(hewa izingike vema kwenye nafasi zote
·         Mlango wa kuingia unapaswa kuwa mkubwa kuliko yote kwenye nyumba.Sababu kubwa ni kuruhusu vitu kuingia na kutoka kama samani na vifaa vingine vikubwaPia nguvu huingia kupitia hapa,hivyo ni muhimu kuingia kwa wingi.

·         Ni muhimu mlango huu wa kuingia ufungukie ndani na kwa mzunguko wa akrabu (clockwise).Sababu kubwa ni kwamba inasaidia kuingia kwa urahisi kwa kusukuma.Pia ni rahisi ukiwa ndani unafungua kwa kutumia mkono wa kushoto na kuwa rahisi kukaribisha ama kuwa tayari kupokea kwa mkono wa kulia.

·         Mlango mkuu unapaswa kuwa na kizingiti.Epuka kuweka viatu mbele ya mlango wa kuingia ndani ya nyumba,sababu ni kuzuia wadudu na wanyama kuingia. Viatu huweza kuvuta wadudu kama nzi, na huweza kusababisha kujikwaa.Pia huleta picha mbaya mbele ya nyumba
·         Mlango mkuu ni muhimu uwe juu kutoka usawa wa ardhi, na kuufikia panapaswa kuwa na ngazi chache kuufikia na zinapaswa kuwa na idadi ya namba witiri. Sababu ya msingi ni kuzuia maji na wanyama wanaotambaa kufikia kirahisi.Pia kuwa juu kutoka usawa wa ardhi kunasababisha taka kutoingia ndani.

Sababu kwa nini ni muhimu kuwa na ngazi chache ambazo idadi yake ni witiri ni kwa sababu watu wengi hutumia mkono wa kulia,huanza kupanda ngazi kwa kunyanya kwanza mguu wa kulia,hivyo anapopanda atamaliza kwa kufika na mguu wa kulia.

·         Mlango mkuu unapaswa kuonekana kwa urahisi na uvutie.Sababu ni kwamba mgeni anapofika anapaswa kuuona kwa urahisi na umvutie(usiwe gizani na usiwe mweusi)
·         Mlango uwe unavutia na ubunifu wa kutosha ikiwemo picha ama alama zenye kuvutia.Bianadamu hupenda kuona vitu vyenye kuvutia

·         Mlango unapaswa utengenezwe zaidi kwa kutumia mbao kwa sababu mbao hudumu nan i rahisi kuweka nakshi na urembo

**ZINGATIA-Mbao inayotumika kutengeneza mlango isitokane na miti isiyokomaa,sitokane na miti inayotoa maua mazuri ya biashara wala harufu kali na isitokane na miti ambayo ipo hatarini kutoweka ili kuzuia upotevu wa miti yenye faida zaidi kwa matunda,maua na yenye historia.
Picha kwa hisani ya mtandao



JE NI MAMBO GANI UNAPASWA KUYAEPUKA UNAPOBUNI MLANGO MKUBWA WA KUINGIA NDANI (AMA KUJENGA)
1.       Kwa nyumba za kuishi epuka mlango wenye kuzunguka (circular door) nay a kutembea (sliding door) kwa sababu kubwa ni kwamba haitoi urahisi katika kutumia na haidumu

2.       Epuka mlango wako mkubwa kuingia kwenye nyumba kutazamana moja kwa moja na mlango mkuu wa nyumba nyingine.Pia mlango usitazamane na msikiti,kanisa ama mahakama. Unapofungua mlango wa nyumba yako mtu huweza kutazama moja kwa moja ndani

3.       Epuka kuwa na miti mikubwa ama kitu kisichohamishika mbele ya mlango wako,utakuzuia kuonavitu vilivyo mbele ya mlango na kisaikolojia  usababisha pingamizi ama vizuizi.

4.       Epuka mlango kutazama moja kwa moja gofu/magofu,unapofungua asubuhi utatazama gofu

5.       Epuka kujenga tanki chini(underground tank) ama tanki la maji taka mbele ya mlango wa kuingia.iwapo itahitajika kusafisha ama kufanya marekebisho itasumbua kupita

6.       Epuka kuweka mlango wa kuingia ndanin ya nyumba kwenye kona ya nyumba.Ni vigumu kupangilia samani kwa sababu kona itatumika kwa ajili ya nafasi ya kutembea.

7.       Epuka kuwa na ukuta unapofungua tu mlango wa kuingia, hewa na mwanga utazuiliwa kupita

8.       Epuka mlango unaojifunga wenyewe. Endapo patakuwa na upepo mkubwa mlango unaweza kujifunga huku funguo zikiwa ndani.

9.       Epuka mlango uliochakaa na unaotoa kelele unapofunguliwa/kufungwa-unaonesha udhaifu wa mlango, uzembe

Je, makala hii imekusaidia kwa njia yoyote? Kama ndio usisite kuwashirikisha wengine kusoma waelimike.
Kwa maswali kuhusu ujenzi usisite kuwasiliana nami
PONGU J- +255 765046644

Sunday, July 19, 2015

KUKAMILISHA NDOTO YA NYUMBA YAKO

Picha ikionesha sehemu za ndani za nyumba kadiri ya muono wa msanifu-Imesanifiwa na P.J



Kila mtu anapotaka kujenga nyumba,huwa na picha ya nyumba aliyenayo.
Uzoefu wangu unaonesha kwamba watanzania wengi huwa hawana muono wa kitu wanachokitaka.Ukikutana na watu wengi wanaohitaji ramani ,huishia kufananisha maono yao na nyumba aliyeiona kwa nje,eitha ya jirani ama rafiki ama mtu maarufu.


Kwa kifupi ningepnda tushirikishane ujuzi kidogo.Ili kuitafsiri ndoto kuhusu kitu unachokitaka ni vizuri kutazama yafuatayo


1.Ukubwa-ukijumuisha,urefu,upana,ukubwa wa vyumba,idadi ya watu watakaotuia nyumba


2.Uhusiano kati ya nafasi moja na nyingine,ni vema picha ulionayo katika fikra zako iwe na tafsiri /picha ya jinsi sehemu moja na nyingine zinavyooana-mfano sebule na dining na vyumba n.k


3. Iwe na picha ya rangi utakazopiga ktka nyumba,kama ni rangi moja ijulikane,kama ni rangi tofauti ijulikane,kama ni aina ya texture ijulikane.Rangi pia ijumlishe ndani,nje,paa


4.Ndoto ni lazima iwe na picha ya jinsi madirisha,milango na vitu vingine vitakavyokuwa.Hii inajumuisha aina ya malighafi itakayotumika,rangi/texturena ukubwa

5.Ni vema ndoto ikawa na picha ya mazingira yanayokuzunguka.Kitu ukiwazacho moyoni mwako huwa.Jinsi unavyofikiri ndivyo unavyokuwa na mazingira huwa vile unavyoyatengeneza.Hivyo kabla ya kuanza kuamua kujenga ni muhimu ukawa na picha ya jinsi mazingira yatakayokuzunguka yatakavyokuwa.Utapaswa kujua bustani inayozunguka,maua,miti ,uoto wake kwa ujumla,majirani


6.Mwisho kabisa tafsiri ya ndoto yako iende kwenye gharama unayotaka kuitumia

Picha kwa hisani ya Pongu J

Nawasilisha na nakaribisha maoni.

Saturday, July 18, 2015

JIPATIE RAMANI-GHOROFA YA KISASA

PLAN DETAILS:
Ground- Sebule kubwa, Dining, Jiko lenye stoo, Laundry, Chumba cha kusalia, chumba cha kusomea( library) na sehemu ya kuegesha gari.
FIRST FLOOR -sEBULE NDOGO, gym,master en suite yenye library,vyumba 2 na ina sehemu kwa ajili ya kupumzika nje kufanya usiyachoke mazingira.
Wasiliana nasi kwa
Email: nyumbaboratz@gmail.com
Mwonekano kwa mbele



Wednesday, July 8, 2015

UCHAGUZI WA RANGI KATIKA NYUMBA

Rangi katika nyumba ina faida kuu mbili,zikiwa ni kuongeza nakshi (kupendezesha ) na kazi ya pili ni kulinda kuta.

unaionaje rangi hii






picha zote ni mali ya Joseph P.

Rangi za kuta zinaweza kuwekwa katika makundi mawili ya rangi msingi na rangi sekondari (upili)
Rangi msingi ni rangi ambazo hupigwa ili kuwezesha rangi upili kudumu.Hujulikana kama primer kwa lugha ya kiingereza

Makala hii fupi inalenga kushirikisha wasomaji na wale ambao wangependa kujenga kuhusu uchaguzi wa rangi.

Ni wazi kuwa kila mtu ana uchaguzi wake wa rangi,na mara nyingi kuvutia kwa rangi ni baina ya mtazamaji na maono yake.

Zipo rangi zilizopoa na zinazong'aa sana.Ni sawa na kusema rangi zinazoakisi zaidi mwanga na zile za kutunza mwanga.

Ndugu msomaji ,nini maoni yako kuhusu rangi za kung'aa na rangi za kupoa.Je wewe binafsi unapenda nyumba yako iweje ukijenga.Kuanzia rangi ya paa mbaka kuta.Unapata picha gani unapofikiri kuhusu nyumba yako?

Niambie wewe umependa rangi ipi kati ya hizo juu.Una maoni gani kwa msanifu wa nyumba hizo hapo juu kuhusu rangi?
Tujadiliane

Friday, July 3, 2015

TUAMBIE HITAJI LAKO

Moja ya sifa ya nyumba ya kisasa ni kuwa na mpangilio wenye kuruhusu nafasi kwa  mahitaji mbalimbali ikiwemo kukaa, chakula, kupumzika, kusomea na kujifunzia,
Sehemu za kupikia, maliwato na pia kuwe na nafasi za kupita na kupitisha vifaa
.Hii ni moja ya nyumba mbayo inakufanya usichoke kuishi.kuna sehemu zote ikiwemo studio na pia nje panatoa nafasi ya mapumziko na kuongeza mvuto wa mazingira.Je hitaji lako ni nini kwenye nyumba?