Kulingana na mapokeo na utaalamu toka kale, ni muhimu sana kuzingatia
pande za dunia unapotaka kujenga,hasa unapochagua sehemu ya kujenga.
Fuatana nami kupitia makala hii uelimike
kuhusu uchaguzi wa eneo la kujenga
Picha ikionesha pande za dunia |
UELEKEO WA KIWANJA
(SITE ORIENTATION)
Uelekeo wa kiwanja maana yake ni mahali(nafasi)
kilipo kiwanja kwa kuzingatia dira. Hutanabaishwa kwa kutazama upande wa mbele
ya kiwanja chako unapotazama.Unaposimsms kwenye kiwanja chako na kutazama ilipo
barabara, upande unaoutazama ndio uelekeo wa kiwanja chako.Kama kiwanja kina
barabara upande wa kaskazini, basi uelekeo wako ni kaskazini(North facing site)
Kutokana na mapokeo zipo pande nane ambazo huzingatiwa kulingana
na lilipo jua.Pande hizi hutokana na pande nne kuu ambazo ni
- Mashariki-Unatambulika ni upande ambao jua huchomoza
- Magharibi-Unatambulika kuwa ni upande jua linapozama
- Kaskazini-Unatazama mashariki,upande ulio kushoto kwako ni Kaskazini
- Kusini-Utazamapo mashariki,upande uliopo kulia kwako ni kusini
Kona ambazo pande mbili kati ya pande
kuu nne zilizotajwa hukutana,ni muhimu kwa sababu kani ya mvutano toka pande
kuu nne huungana.
- Kaskazini mashariki-Ni upande ambao pande mbili za kaskazini na mashariki zinakutana Kaskazini Magharibi-Ni upande ambao pande mbili za kaskazini na magharibi zinakutana
- Kusini Magharibi-Ni upande ambao pande mbili za kusini na magharibi zinakutana
- Kusini Mashariki-Ni upande ambao pande mbili za kusini na mashariki zinakutana
-
KWA NINI MWELEKEO WA KIWANJA NI MUHIMU SANA
WAKATI WA KUCHAGUA KIWANJA CHAKO?
Jua ni muhimu sana katika maisha ya
viumbe hai.
Jua husababisha mimea kujitengenezea chakula chake,ambayo baadae
wanadamu hula.Jua husaidia mwili wa binadamu kutengeneza Vitamini D.Jua pia
huleta nuru.Kwa kifupi ni vigumu kutofautisha jua na uhai wa viumbe.Ukiachilia
mbali faida za jua,pia zipo hasara kwa viumbe,akiwwemo binadamu
Hivyo ni muhimu wakati wa kupangilia nyumba, ni muhimu kuhakikisha
binadamu anahakikishiwa miale ya jua yenye faida na kukingwa na miele mikali ya
jua yenye madhara.Vymba na nafasi zote zinazohitajika kwenye nyumba ni lazima
zipangiliwe kuhakikisha zinapata mwanga wa jua wenye faida na kukingwa na miale
yenye kuleta athari
Mwelekeo wa nyumba yako kuzingatia mawio na machweo ya jua ni muhimu |
JE NI UPANDE UPI MZURI KWA KIWANJA CHAKO?
Pande zote zinafaa,zikiwa zina faida na
hasara yake.Mpangilio wa mji huzingatia uwepo wa barabara katika pande zote za
mtaa(Kwa maeneo yaliyopangiliwa tu) na pande zote huhitajika kuwepo
majengo(nyumba) ili kufanya mtaa(mji) uvutie na kufikika kwa urahisi
KIWANJA KINACHOTAZAMA MASHARIKI
Upande huu ndipo jua linapochomoza.Miale
yenye faida huwa jua linapochomoza.Utafiti unaonesha jua la majira ya saa
nne(asubuhi) husaidia mwili kuzalisha vitamin D.Hivyo kiwanja kitazamacho
upande huu hutoa nafasi nzuri zaidi kupangilia nafasi zako katika nyumba,hasa
ikitazama upande huu. Ukiamka unakutana na mwanga wa jua unaochochea ubongo
kufanya kazi vema.Katika baadhi ya tamaduni upande huu huhusishwa na ucha
Mungu, uaminifu, elimu na ibada.
UPANDE WA KASKAZINI
Upande huu una uhusiano mzuri na kuvuma
kwa upepo na miale ya jua.Katika imani mbalimbali kiwanja kitazamacho Kaskazini
huhusiana na nguvu na utawala
UPANDE WA KUSINI
Mara nyingi viwanja vyeye kutazama
upande huu havipendelewi sana kwa sababu huhitaji zaidi umakini katika
kupangilia nyumba yako na mazingira yanayohusiana na nyumba yako.Viwanja hivi
hufaa zaidi kwa matumizi ya biashara kuliko ya makazi.
UPANDE WA MAGHARIBI
Ni upande jua linapozama.
Ni muhimu kuwa makini unapopangilia
nyumba yako kwa kiwanja kitazamacho upande huu
Je Makala hii imekusaidia kujifunza chochote?Kama ndio washirikishe wengine waelimike.
Usisite kuniandikia maoni yako na maswali kuhusu ujenzi.
1 comment:
Ahsante kwa uelewa huu hakika nimejifunza kitu muhimu.
Post a Comment