1.MLANGO MKUBWA WA KUINGIA NDANI(MAIN
DOOR)
picha kwa hisani ya Pongu J |
Mlango mkuu wa kuingia kwenye
nyumba ndio unaokaribisha anayeingia ndani.Kiimani ni lango la kukaribisha
nguvu zote zenye faida na zenye madhara.Pia ni mlango mkuu wa kutoka ndani ya
nyumba.
·
Ni muhimu mlango wa kuingia
ndani uoane ama uwe katika uelekeo mmoja na lango kuu la kuingia (Gate)
·
Lango kuu(gate) na mlango wa kuingia ndani ni vema view upande
mmoja. Sababu kubwa ni kufanya kuwa na urahisi kuingia lango kuu na kutembea
moja kwa moja kwenda kwenye mlango wa nyumba pasipo kuzinguka.Pia ni rahisi
kujua anayeingia na kutoka
·
Mlango mkuu wa kuingia ni
muhimu uwe mkubwa na iwe miwili(double door) yaani ufunguke sehemu mbili.
Pia ni muhimu nyumba kuwa na milango miwili ya nje kuruhusu kuingia na kutoka kwa urahisi pale inapohitajika, na kufanya hewa kuingia na kutoka na kuufanya mzunguko wa hewa ndani ya nyumba
·
Upande wa kuingia unapaswa
kuwa mkubwa kuliko wa kutoka.Sababu kubwa ni kwamba,hapa ndipo hewa(air)
inavuma kutoka nje kwenda ndani.Unapaswa iignie kwa wingi na kutoka kidogo
kufanya nyumba ipumue(hewa izingike vema kwenye nafasi zote
·
Mlango wa kuingia unapaswa
kuwa mkubwa kuliko yote kwenye nyumba.Sababu kubwa ni kuruhusu vitu kuingia na
kutoka kama samani na vifaa vingine vikubwaPia nguvu huingia kupitia hapa,hivyo
ni muhimu kuingia kwa wingi.
·
Ni muhimu mlango huu wa
kuingia ufungukie ndani na kwa mzunguko wa akrabu (clockwise).Sababu kubwa ni
kwamba inasaidia kuingia kwa urahisi kwa kusukuma.Pia ni rahisi ukiwa ndani
unafungua kwa kutumia mkono wa kushoto na kuwa rahisi kukaribisha ama kuwa
tayari kupokea kwa mkono wa kulia.
·
Mlango mkuu unapaswa kuwa na
kizingiti.Epuka kuweka viatu mbele ya mlango wa kuingia ndani ya nyumba,sababu
ni kuzuia wadudu na wanyama kuingia. Viatu huweza kuvuta wadudu kama nzi, na
huweza kusababisha kujikwaa.Pia huleta picha mbaya mbele ya nyumba
·
Mlango mkuu ni muhimu uwe
juu kutoka usawa wa ardhi, na kuufikia panapaswa kuwa na ngazi chache kuufikia
na zinapaswa kuwa na idadi ya namba witiri. Sababu ya msingi ni kuzuia maji na
wanyama wanaotambaa kufikia kirahisi.Pia kuwa juu kutoka usawa wa ardhi
kunasababisha taka kutoingia ndani.
Sababu kwa nini ni
muhimu kuwa na ngazi chache ambazo idadi yake ni witiri ni kwa sababu watu
wengi hutumia mkono wa kulia,huanza kupanda ngazi kwa kunyanya kwanza mguu wa
kulia,hivyo anapopanda atamaliza kwa kufika na mguu wa kulia.
·
Mlango mkuu unapaswa
kuonekana kwa urahisi na uvutie.Sababu ni kwamba mgeni anapofika anapaswa
kuuona kwa urahisi na umvutie(usiwe gizani na usiwe mweusi)
·
Mlango uwe unavutia na
ubunifu wa kutosha ikiwemo picha ama alama zenye kuvutia.Bianadamu hupenda
kuona vitu vyenye kuvutia
·
Mlango unapaswa utengenezwe
zaidi kwa kutumia mbao kwa sababu mbao hudumu nan i rahisi kuweka nakshi na
urembo
**ZINGATIA-Mbao
inayotumika kutengeneza mlango isitokane na miti isiyokomaa,sitokane na miti
inayotoa maua mazuri ya biashara wala harufu kali na isitokane na miti ambayo
ipo hatarini kutoweka ili kuzuia upotevu wa miti yenye faida zaidi kwa
matunda,maua na yenye historia.
Picha kwa hisani ya mtandao |
JE NI MAMBO GANI UNAPASWA KUYAEPUKA
UNAPOBUNI MLANGO MKUBWA WA KUINGIA NDANI (AMA KUJENGA)
1.
Kwa nyumba za kuishi
epuka mlango wenye kuzunguka (circular door) nay a kutembea (sliding door) kwa
sababu kubwa ni kwamba haitoi urahisi katika kutumia na haidumu
2.
Epuka mlango wako mkubwa
kuingia kwenye nyumba kutazamana moja kwa moja na mlango mkuu wa nyumba
nyingine.Pia mlango usitazamane na msikiti,kanisa ama mahakama. Unapofungua
mlango wa nyumba yako mtu huweza kutazama moja kwa moja ndani
3.
Epuka kuwa na miti
mikubwa ama kitu kisichohamishika mbele ya mlango wako,utakuzuia kuonavitu
vilivyo mbele ya mlango na kisaikolojia
usababisha pingamizi ama vizuizi.
4.
Epuka mlango kutazama
moja kwa moja gofu/magofu,unapofungua asubuhi utatazama gofu
5.
Epuka kujenga tanki
chini(underground tank) ama tanki la maji taka mbele ya mlango wa kuingia.iwapo
itahitajika kusafisha ama kufanya marekebisho itasumbua kupita
6.
Epuka kuweka mlango wa
kuingia ndanin ya nyumba kwenye kona ya nyumba.Ni vigumu kupangilia samani kwa
sababu kona itatumika kwa ajili ya nafasi ya kutembea.
7.
Epuka kuwa na ukuta
unapofungua tu mlango wa kuingia, hewa na mwanga utazuiliwa kupita
8.
Epuka mlango unaojifunga
wenyewe. Endapo patakuwa na upepo mkubwa mlango unaweza kujifunga huku funguo
zikiwa ndani.
9.
Epuka mlango uliochakaa
na unaotoa kelele unapofunguliwa/kufungwa-unaonesha udhaifu wa mlango, uzembe
Je, makala hii imekusaidia kwa njia
yoyote? Kama ndio usisite kuwashirikisha wengine kusoma waelimike.
Kwa maswali
kuhusu ujenzi usisite kuwasiliana nami
PONGU J- +255 765046644
No comments:
Post a Comment