Kutafuta kiwanja ni hatua ya awali kabisa kuelekea
kujenga nyumba ya ndoto yako. Hatua hii ni muhimu sana kwani ardhi ni gharama
na ukishajenga, kubadili maamuzi huleta gharama kubwa zaidi.
Fuatana nami katika makala hii ili uweze kufuhamu ni
mambo gani muhimu katika uchaguzi wa kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba ya
makazi.
Kwa kifupi, nyumba ya kuishi inapaswa kuwa ni sehemu
yenye utulivu , amani, uoto mzuri na ijengwe sehemu yenye urahisi wa upatikanaji wa huduma
muhimu kama maji,usafiri na yenye kuleta msawazo wa mawazo. Pia kila binadamu
hupenda amani ,hivyo ni muhimu uchaguzi
wa kiwanja uzingatie dhana hii.
Yafuatayo ni mambo ya msingi unayopaswa kutilia
mkazo unapochagua eneo la kujenga
1.
Imani
yako kwanza ni muhimu. Inashauriwa usimame kwenye eneo unalotaka kununua ksha
sikiliza mvuto wa eneo hilo.Kama panakuvutia moyo wako utakuvutiwa nalo,kama
hapana,utakuwa na mashaka nalo
2. Chunguza
historia ya eneo unalotaka kununua.
Unashauriwa kununua eneo lenye historia njema kwa
jamii iliyopita kabla yako.Iwe ni sehemu ambayo watu walioishi walikuwa na
furaha ,amani na umoja.Sababu kubwa ya kuchunguza ni kwamba kuna uhusiano
mkubwa sana wa kimaendeleo kati ya watu walioishi awali na namna ardhi
ilivyotumika.Kuishi sehemu yenye watu wenye amani,upendo na mshikamano
kutakufanya wewe na kizazi chako uishi pia kwa amani ,upendo na mshikamano.
3. Kiwanja
ambacho kinafikika.
Kiwanja chenye barabara pande zote huhusiana na
furaha, afya njema na mafanikio. Huwa na hewa, mwanga na nafasi ya kutosha
Kwa kiwanja kisichokuwa na barabara pande zote,ni
muhimu kiwe na barabara kwa upande wa kaskazini ama Mashariki mwake.Sababu ya
msingi ni ni kwamba nyumba itakayojengwa itakuwa na mwanga na hewa ya kutosha
kuanzia asubuhi.
Katika sehemu za Asia hasa India,kiwanja chenye maji
upande wa kaskazini ama mashariki hupendelewa zaidi,sababu ikiwa ni uwezekano
mkubwa wa kuwepo mwanga,hewa na mandhari ya kutosha na kwamba miale ya jua ya
asubuhi(Ultraviolet light ) husaidia kuua vijidudu kwenye maji na kuyafanya
yafae kutumika
4.
Hakikisha eneo unalonunua
ni la makazi ama makazi na biashara.
Itakufanya uepuke na usumbuufu kubomolewa ama kuwa
na hofu ya kuhamishwa.Hakikisha unafuata taratibu zilizowekwa katika kumiliki
ardhi.
Nyumba iliyozungukwa na maji upanse wa mashariki.Picha kwa msaada wa architectureideas.com |
Je
ni kiwanja cha namna gani hakikufai katika ujenzi wa makazi?
1. Epuka
kiwanja kinachouzwa na mtu aliyepatwa na dhiki/filisika
Kiwanja cha namna hii ni muhimu kinunuliwe kwa
uangalifu mkubwa kwa kuzingatia kumwinua mwenye dhiki ama shida.
Ununuzi wa kiwanja cha namna hii kwa malengo ya
kujinufaisha wewe zaidi kitakufanya baadae ukose furaha na amani na labda
manung’uniko yatokanayo na muuzaji ama jamii inayozunguka yanaweza kukuondolea
heshima na utu.
2. Epuka
kiwanja kilicho jirani/kinachopakana na
maeneo ya mikusanyiko mikubwa ya kijamii.
Maeneo haya ni kama kumbi za starehe, kanisa,
msikiti , kiwanda, chuo, jeshini, shule,
soko, sehemu stesheni za magari.
Maeneo haya huwa na kelele nyingi na mara nyingi matumizi ya maeneo haya
huadhiri maeneo yaliyo jirani,ikiwemo kubadilishwa kwa matumizi wakati
wowote.Ni vigumu kulea watoto na kuwakuza kimaadili katika maeneo yaliyojirani
na sehemu nilizozitaja hapo juu.
3. Epuka
kununua eneo linalomilikiwa ama lililomilikiwa na taasisi za kiimani.
Wengi wanaweza wasielewe hili. Wakati wowote taasisi
za kiimani huweza kuuza maeneo kwani ni
haki yao ya msingi. Lakini kadiri mahitaji yanapoongezeka miaka kwa
miaka,uwezekano mkubwa wa kulihitaji eneo lao la awali hujitokeza.Kwa sababu ni
vigumu kushindana na taasisi, ni ukweli usiopingika kwamba mazingira
yatakufanya ulazimike kuondoka na kuanza maisha upya,licha ya kwamba utalipwa.
4. Epuka
eneo lililo jirani na sehemu za taka na zenye harufu kali.
Kiwanja chako hakipaswi kuwa jirani na machinjio,
mashimo ya taka ngumu na maji taka, mitaro mikubwa ya maji, sehemu
wanapotengeneza na kuuza viatu, tairi kwa wingi.
Meneo haya kwa wakati wote yanaweza yakawa na harufu
kali na kufanya usiishi kwa furaha na amani.
5. Epuka
kununua kiwanja eneo lenye magofu mengi.
Zipo sehemu ambazo zina magofu mengi yatokanayo na
sababu mbalimbali.Mara nyingi maeneo haya huwa ni kivutio cha vibaka, majambazi
na wanyama wakali. Kuishi maeno haya huzua hofu.
eneo lenye magofu(picha kwa msaada wa mtandao) |
6.
Epuka kiwanja kilichopo
eneo lenye dungusi (kakati) (jamii ya mimea kama mpungate.
Sababu ya msingi ni kwamba maeneo yenye mimea hii
huwa na udongo dhaifi usio rafiki kwa msingi wa nyumba yako.
7. Epuka
kiwanja kilicho sehemu yenye mchwa na
kumbikumbi wengi
Sababu kubwa ni kwamba ni vigumu kuyaondoa makazi ya
mchwa. Mchwa huharibu mbao na hata kudhoofisha msingi na kuta za nyumba. Pia
huweza kushambulia samani mbalimbali.
8. Epuka
kiwanja kidogo kilichozungukwa na viwanja vikubwa.
Sababu kubwa ni kwamba mmiliki wa kiwanja kidogo
hulazimika kujenga nyumba ndogo ,na wamiliki wa viwanja vikubwa hujenga nyumba kubwa na kuwa na matumizi
mengi zaidi kwenye eneo moja, hivyo mmiliki wa nyumba ndogo (kiwanja
kidogo) hushawishika kujitazama kama
mnyonge na mara nyingi hudhani anaonewa(inferiority complex)
9.
Epuka kiwanja chenye
mapingamizi ya milima,mabonde na majengo marefu hasa upande wa mashariki na
kaskazini mwa kiwanja.
Sababu kubwa
ni kwamba majengo marefu na
milima/mabonde huzuia hewa ya kutosha ,mwanga na huweka kivuli (giza) kwenye
nyumba.
Habari njema ni kuwa kiwanja kilicho na milima ama majengo
marefu upande wa kusini na upande wa magharibi husaidia kuzuia miale mikali ya
mwanga.
10. Epuka
kiwanja kilicho na nguzo kubwa za umeme
kwenye kona ya kaskazini-mashariki.
Sababu kubwa ni kwamba umeme unaopita kwenye nguzo
huwa na mawimbi (electrical waves) ambazo huwa na madhara na ukubwa wa nguzo
huzuia mwanga na hewa kufikia nyumba itakayojengwa.
11. Epuka
kiwanja chenye nyufa/mipasuko(cracks) na udongo wenye mfinyanzi.
Nyufa kwenye ardhi huwa na uhusiano mkubwa na udongo
wa mfinyanzi unaoruhusu maji mengi kutuama.Udongo huu si rafiki kwenye ujenzi
na huhitaji gharama kubwa kujenga msingi.
12. .Epuka
kiwanja chenye miti mingi yenye mizizi mirefu na minene
Kama kiwanja unachotaka kujenga ni kidogo na kina miti mingi yenye mizizi
mikubwa na minene inayotambaa,si vema kukinunua kwa sababu mzizi hukua na
kusababisha nyufa kwenye msingi na hata kufikia kuta za nyumba
13. Epuka
kiwanja kilichopo kwenye makutano ya barabara kuu hasa makutano yenye
kutengeneza herufi T ama Y.
Kiwanja kilichopo kwenye makutano huwa na kelele
nyingi, vumbi na wakati Fulani huondoa sitiri(privacy). Makutano yenye
kutengeneza herufi T ama Y kuielekea
nyumba (kiwanja) ni rahisi kutokea ajali hasa kwa magari kugongana, watu
kugongwa wakati wa kuvuka na pia heleta hofu ya kudhani gari zitagonga nyumba.
nyumba iliyojengwa kwenye kiwanja kilicho kwenye makutano ya barabara |
14. Epuka
kiwanja chenye umbo la duara,sambusa ama pembetatu.
Kiwanja cha namna hii kama si kikubwa huongeza ugumu
katika kuongeza matumizi na kujenga nyumba yenye ukubwa wa kutosha.Katika imani
Fulani viwanja vyenye umbile la duara na pembetatu huhusianishwa na huzuni,
umasikini na magonjwa.
Ahsante.
Makala imeandaliwa na Pongu J
+255 717 903089, +255 765046644
No comments:
Post a Comment