Thursday, July 27, 2023

TUNATOA HUDUMA YA INTERIOR DESIGN

 Tunapenda kuwatangazia kuwa kwa sasa tunatoa pia huduma ya Interior Design

Tunadesign, kutengeneza na kushauri yafuatayo

-Majiko ya kisasa(Kitchen Cabinets)

-Kabati za nguo 

-Sebule, Vyumba ikiwemo mwonekano wake, Rangi, mapambo (decoration)

Zifuatazo ni badhi ya kazi zetu

Kwa kazi hizi tupigie kwa namba 0717903089  (Whatsapp pia), Email  nyumbaboratz@gmail.com





NYUMBA YA KISASA YA VYUMBA 3

Hii ni  nyumba ya kisasa iliyosanifiwa kukidhi mahitaji ya vyumba 3,sebule, dining, jiko la kisasa lenye stoo na laundry.

Inaweza kujengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa meta 20 kwa 25.Ina sehemu ya kupack gari.
Wasiliana nasi kwa 0717903089 ama Email: nyumbaboratz@gmail.com




NYUMBA YA KISASA YA VYUMBA 4

 Hii  ni design ya nyumba ya kisasa yenye vyumba 4.

Imesanifiwa vema kuzingatia  mahitaji ya mteja ambaye angependa kuwa na nyumba yenye sitiri, nafasi ya kutosha.

Pia ina chumba kidogo cha kusomea.





Saturday, April 28, 2018

FANGASI(KUVU ) KWENYE NYUMBA NA NAMNA YA KUONDOA TATIZO

Katika Makala hii tutajadili tatizo linalozikumba nyumba nyingi kwenye sehemu za unyevu, ambalo ni la kuta,ceiling, madirisha, sakafu, msingi na hata milango kushambuliwa na fangasi.
dari iliyoathiriwa na fangasi



SABABU ZA KUOTA FANGASI KWENYE KUTA
Sababu kuu ya kutokea kwa fangasi kwenye kuta ni Unyevunyevu , kuganda kwa maji na  kuvuja kwa maji toka kwenye mabomba yaliyopasuka ama kupata ufa.

Kuganda kwa maji hutokea pale mvuke unapokutana na hewa/kitu cha baridi kisha kupoozwa na kuwa maji. Kama kuganda kutachukua muda mrefu kwenye kuta,fangasi huanza kukua kwenye kuta


Mabomba ya maji kwenye nyumba yanapopasuka ama kupata ufa,huruhusu maji kutiririka kenye msingi na kuta.Maji haya hulowesha kuta na msingi na kusababisha kuzaliana kwa fangasi.Fangasi huweza kuonekana kwenye sehemu mbalimbali za nyumba yako kama ifuatavyo

Fangasi kwenye Dari
Hutokana na  unyevunyevu kwenye dari unaoweza kusababishwa na kuvuja kwa maji ama kuganda kwa maji.
Fangasi kwenye Milango na madirisha
Unyevu kwenye madirisha husababisha kutokea kwa fangasi.
Fangasi kwenye sakafu
Unyevu kqwenye sakafu nhusababisha kukua kwa fangasi.Sehemu nyingi ambazo maji hayakauki,hupanda kwenye msingi na kuingia kwenye sakafu.Ni muhimu sana kuhakikisha hatua za awali za kudhibiti unyevu kuingia kwenye sakafu zinatiliwa mkazo.
Fangasi kwenye kuta

Unyevu unapopanda kwenye kuta husababisha fangasi kutokua.Kadiri kuta zinzvyoathiriwa na maji(unyevu) ndivyo fangasi zinavyokuwa.
Kwenye kuta zinye karatasi(wall paper) Na hata nguo hushambuliwa


 Dalili za fangasi kwenye kuta na sehemu mbalimbali
Zifuatazo ni dalili kuwa ukuta wako ama nyumba yanko inashambuliwa na fangasi
1.Kubadilika kwa rangi ya kuta kuwa nyeusi ama kijani
2.Kubanduka kwa rangi ya nyumba na nkubadilika
3.Unyevu wa muda mrefu kwenye kuta/sakafu
4.Kutokea kwa alama zenye rangi nnyeusi kwenye kuta/sakafu
5.Kutokea kwa harufu ya uyoga inayoweza kusababisha mafua ama chafya
Muhimu: Kuzaliana kwa fangasi kwenye nyumba yako husababisha madhara makubwa ya kiafya kwa wanaoishi kwenye nyumba na pia hudhoofisha kuta, rangi,sakafu na hata kuifanya nyumba isiwe imara
Fangasi pia hutokea sana kwenye bafu na vyoo kutokana na unyevu wa mara kwa mara, hivyo ni muhimu sehemu hizi kutiiwa mkazo zaidi.
madoa meusi ni dalili ya kuota fangasi kwenye ukuta


UNAWEZAJE KUONDOA FANGASI KWENYE NYUMBA YAKO(KUTA/SAKAFU)
Kabla ya kujadili namna ya kuondoa fangasi kwenye nyumba yako,ni muhimu kuzingatia hatua ya awali ya kuzuia kabisa kutokea kwa unyevunyevu ama maji kwenye kuta/sakafu kwa muda mrefu.
Ni muhimu wakati unajenga kwenye sehemu yenye unyevu unaotoka ardhini kutumia njia za kuzuia unyevu kupanda kwenye kuta ama msingi.Tumia Damp roofing membrane/course.Ni muhimu kuzingatia maoni ya wataalamu wakati wa kujenga.
Kama tayari umejenga kwenye sehemu yenye unyevu,waite wataalamu watazame namna bora ya kudhibiti unyevu kwenye eneo lako(nyumba yako)
Kama kuna mabomba yanayovuja,zingatia kuyaziba
Kama bati lako linavuja,zingatia kiuziba


Zipo njia nyingi za kuondoa fangasi kwenye nyumba za asili na za kutumia kemikali. Ni muhimu kuanza na njia za asili kwanza kabla ya kutumia kemikali kuondoa tatizo.Njia hizi hutofautiana kulingana na ukubwa wa tatizo na pia kulingana na sehemu iliyoathiriwa.
·         Kwenye kuta zenye rangi ni muhimu kuondoa kabisa tabaka la rangi lililoathiriwa. Hakikisha unakwangua rangi yote iliyoathiriwa na kuiondoa.
·         Kisha chukua siki nyeupe, robo kikombe ,changanya kwenye maji moto sana lita 2 pamoja na borax vijiko viwili . Koroga vyema mchanganyiko wako. Kisha safisha ukuta wako sehemu iliyoathiriwa na fangasi.Futa kwa kitambaa kama ni ukuta wenye rangi.Fangasi itaondoka.
·         Kwa sehemu ambazo fangasi imeathiri sana tumia dawa ya kuoindoa fangasi(Bleach Based mold remover)
Muhimu kuzingatia ni kwamba njia hii huondoa fangasi iliyopo lakini si kuzuia mazalia mapya hivyo ni muhimu sana kuchukua hatua kwanza kudhibiti unyevu kwenye nyumba yako
Mahitaji
-Robo kikombe cha bleach
Lita 2 ya maji moto
Changanya mchanganyiko wako vema kisha nyunyuzia kwenye sehemu iliyoathiriwa na fangasi
Rudia kunyunyuzia baada ya dakika 15.Kaa baada ya siku 2 na kunyunyuzia tena
(Hakikisha ukuta wako ni mkavu
·         Hakikisha unasafisha vema kuta za bafu na vyoo kwa kutumia dawa yenye siki kama iliyooneshwa hapo juu.Fungua madirisha kwa dakika 15 unapooga ama kutumia bafu. Anika taulo kwenye jua unapolitumia kuzuia kuota kwa fangasi
·         Kama kuta za nyumba hasa za ndani zimeathiriwa sana,badili kuta kwa kutumia vifaa(material) isuiyoathiriwa kwa urahisi na fangasi kama vioo,plastic,kuta za aluminiam na vioo
·         Iwapo sakafu imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na unyevu haukomi,ita wataalamu wabadili sakafu huku wakidhibiti unyevu huku wakitumia vifaa visivyoathiriwa kwa urahisi na unyevu kama tiles(marumaru) ama terrazzo.
·         Kwa rangi za kuta tumia rangi zinastahimili unyevu na fangasi(anti moulds paints),pia tumia lipu inayoweza kustahimili unyevu(anti-mould plaster)
·         Tumia rangi msingi(primer) inayozuia unyevu(barrier primer/anti-mould primer)
·         Iwapo unatumia wall paper(karatasi za kubandika ukutani) hakikisha unaondoa kwanza fangasi kwa kutumia njia iliyotajwa ha[po juu kisha acha ikauke na kubandika karatasi yako
·         Usiweke samani kuegemea ukuta ulioathiriwa na fangasi






Je Makala hii imekusaidia?
Wailiana nami Pongu J
0765046644

Saturday, April 14, 2018

ELIMU KUHUSU MABATI






Makala hii nimeiandaa ili kukuelimisha elimu ya kawaida na muhimu kuhusu mabati,ikiwemo maneno yanayotumika kwenye bati, hivyo sitaingia kwa kina sana kuhusu namna bati linavyoundwa.Lengo ni kukuelimisha na kukufanya uweze kufahamu mambo muhimu kabla ya kuchagua na kununua bati kwa ajili ya kuezeka nyumba yako.
Katika miaka ya hivi karibuni mabati yamekuwa yakitumika zaidi katika kuezekea katika nchi za Afrika.Umuhimu wake unatoa sababu za kutosha ya wanaotaka kujenga kujifunza kwa kina kuhusu mabati na namna ya kuchagua.

Mabati hutengenezwa kutokana na metali mbalimbali ikiwemo chuma,aluminium,zinc,kopa ama mchanganyiko kati ya metali mbalimbali ambao hujulikana kama aloi(Alloy)
Alloy hutumika kupunguza eitha udhaifu Fulani ama kupunguza gharama ya kutengeneza bati.Mfano bati linalotengenezwa kwa aluminium pekee ni imara zaidi na halipati kutu,lakini ni gharama sana.Hivyo kupunguza gharama,huongezwa madini ya chuma ama zinc ama tin.
Mfano mwingine ni kwamba mabati yanayotengenezwa kwa chuma na zinc hupata kutu mapema,hasa sehemu zenye unyevu mwingi na chumvichumvi hivyo kiwango cha kimojawapo kati ya zinc na chuma kipunguzwe kudhibiti.
Ni muhimu kujikumbusha yafuatayo:-



2. Aluminium haishiki kutu,inadumu hivyo mabati yaliyotengenezwa kwa 100% aluminium yana ubora .Bei yake ni kubwa ukilinganisha na mabati yatokanayo na chuma ama mchanganyiko wa chuma na madini mengine.


3. Aluminum ikitengenezewa bati zinazotumika mikoa ya pwani hudumu Zaidi


4. Pia bati za aluminium zinafaa kwa sehemu zenye unyevu na chumvichumvi ambako mabati ya metali zingine hupata kutu na kuoza


5. Kopa(copper) hutoa mabati yanayoweza kudumu zaidi ya miaka mia moja.Kutokana na kopa kuwa na gharama kubwa ni wachache huweza kununua,na pia viwanda vingi havitengenezi mabati haya kutokana na kukosa wateja.


6. Mabati yaliyotengenezwa kwa kutumia aluminium na zinc huitwa ALU-ZINC.Neno galvanised humaanisha madini yamepakwa kwenye kitu. Mfano chuma kupakwa zinc kuifanya isipate kutu mapema


7. Zinc pia ni madini aghali,hivyo ni nadra kukuta imetumika kutengeneza bati pasipo kuongezwa na madini mengine


8. Mabati yanayoandikwa Coated humaanisha yamepakwa madini mengine kuzuia kutu(tambua kupaka ni tofauti na alloy)


9. Mabati yanayotokana na mabati ya aluminium,zinc na coppey hayahitaji kupakwa madini mengine kwa sababu ya uwezo wa madini hayo kuhimili unyevu na chumvi chumvi


10. Mabati ambayo ni galvanised na galvalume(yaani yatokanayo na mchanganyiko wa chuma na zinc ama chuma na aluminium hayahitaji kupaka trangi juu yake kwa sababu ya mchanganyiko wake ambao ni PRE-COATED



11. Mabati ambayo ni coated yaani yaliyopakwa rangi juu yake,ni muhimu kuhakikisha rangi iliyotumika ni ile itokanayo na mimea kama Kynar 500 tofauti na yale ambayo hupakwa rangi za Acrylic


GAUGE/GEJI
Wengi tumekuwa tukisikia neon geji lakini tusijue maana yake.
Unapozungumzia geji unazungumzia nkina cha bati (yaani Unene wa bati)Bati inapotengenezwa kiwandani,mchanganyiko wake huthibitiwa kwenye kipimo kinachohakiki mchanganyiko unakuwa na kina(unene) unaotakiwa



Kipimo kinachopima unene wa bati husomeka katika namba ndogo bati linapokuwa nene,mfano geji namba 26 ni nene kuliko geji namba 28 nani nene kuliko geji namba 30.Hivyo bati nene ni geji namba 26.


Unene wa bati una uhusiano mkubwa na ubora.Bati geji namba 26 ni bora zaidi kuliko namba 28.Bati geji namba 28 ni bora kuliko namba 30.


Kadiri unene unavyoongezeka ndivo madini ya aluminium huwa mengi zaidi hivyo unapoenda kuchagua bati chagua geji yenye namba ndogo zaidi kama 26,28.


Bei ya geji namba 26 kwa madini yaleyale ni kubwa kuliko namba 28
Bati nyingi huanza gauge 22(22GA)



Mabati yanapotengenezwa hutoka yakiwa hayana mikunjo.Huwa yamenyoka.Kisha huwekwa mikunjo ili kulifanya kuwa imara(lisilokunjikakunjika).Hapo huitwa corrugated,yaani lina mikunjo/migongo

IT 4/IT5
Wengi pia wamekuwa wakiuliza maana ya maneno haya IT5/IT6
Neno IT huwakilisha Industrial Trough,yaani kwa kifupi ni sawa na kusema mikunjo.Inapokuwa na mikunjo 4 huitwa IT4,inapokuwa 5 inaitwa IT5.


Nawasilisha-Niite Pongu J-0765046644