Saturday, April 28, 2018

FANGASI(KUVU ) KWENYE NYUMBA NA NAMNA YA KUONDOA TATIZO

Katika Makala hii tutajadili tatizo linalozikumba nyumba nyingi kwenye sehemu za unyevu, ambalo ni la kuta,ceiling, madirisha, sakafu, msingi na hata milango kushambuliwa na fangasi.
dari iliyoathiriwa na fangasi



SABABU ZA KUOTA FANGASI KWENYE KUTA
Sababu kuu ya kutokea kwa fangasi kwenye kuta ni Unyevunyevu , kuganda kwa maji na  kuvuja kwa maji toka kwenye mabomba yaliyopasuka ama kupata ufa.

Kuganda kwa maji hutokea pale mvuke unapokutana na hewa/kitu cha baridi kisha kupoozwa na kuwa maji. Kama kuganda kutachukua muda mrefu kwenye kuta,fangasi huanza kukua kwenye kuta


Mabomba ya maji kwenye nyumba yanapopasuka ama kupata ufa,huruhusu maji kutiririka kenye msingi na kuta.Maji haya hulowesha kuta na msingi na kusababisha kuzaliana kwa fangasi.Fangasi huweza kuonekana kwenye sehemu mbalimbali za nyumba yako kama ifuatavyo

Fangasi kwenye Dari
Hutokana na  unyevunyevu kwenye dari unaoweza kusababishwa na kuvuja kwa maji ama kuganda kwa maji.
Fangasi kwenye Milango na madirisha
Unyevu kwenye madirisha husababisha kutokea kwa fangasi.
Fangasi kwenye sakafu
Unyevu kqwenye sakafu nhusababisha kukua kwa fangasi.Sehemu nyingi ambazo maji hayakauki,hupanda kwenye msingi na kuingia kwenye sakafu.Ni muhimu sana kuhakikisha hatua za awali za kudhibiti unyevu kuingia kwenye sakafu zinatiliwa mkazo.
Fangasi kwenye kuta

Unyevu unapopanda kwenye kuta husababisha fangasi kutokua.Kadiri kuta zinzvyoathiriwa na maji(unyevu) ndivyo fangasi zinavyokuwa.
Kwenye kuta zinye karatasi(wall paper) Na hata nguo hushambuliwa


 Dalili za fangasi kwenye kuta na sehemu mbalimbali
Zifuatazo ni dalili kuwa ukuta wako ama nyumba yanko inashambuliwa na fangasi
1.Kubadilika kwa rangi ya kuta kuwa nyeusi ama kijani
2.Kubanduka kwa rangi ya nyumba na nkubadilika
3.Unyevu wa muda mrefu kwenye kuta/sakafu
4.Kutokea kwa alama zenye rangi nnyeusi kwenye kuta/sakafu
5.Kutokea kwa harufu ya uyoga inayoweza kusababisha mafua ama chafya
Muhimu: Kuzaliana kwa fangasi kwenye nyumba yako husababisha madhara makubwa ya kiafya kwa wanaoishi kwenye nyumba na pia hudhoofisha kuta, rangi,sakafu na hata kuifanya nyumba isiwe imara
Fangasi pia hutokea sana kwenye bafu na vyoo kutokana na unyevu wa mara kwa mara, hivyo ni muhimu sehemu hizi kutiiwa mkazo zaidi.
madoa meusi ni dalili ya kuota fangasi kwenye ukuta


UNAWEZAJE KUONDOA FANGASI KWENYE NYUMBA YAKO(KUTA/SAKAFU)
Kabla ya kujadili namna ya kuondoa fangasi kwenye nyumba yako,ni muhimu kuzingatia hatua ya awali ya kuzuia kabisa kutokea kwa unyevunyevu ama maji kwenye kuta/sakafu kwa muda mrefu.
Ni muhimu wakati unajenga kwenye sehemu yenye unyevu unaotoka ardhini kutumia njia za kuzuia unyevu kupanda kwenye kuta ama msingi.Tumia Damp roofing membrane/course.Ni muhimu kuzingatia maoni ya wataalamu wakati wa kujenga.
Kama tayari umejenga kwenye sehemu yenye unyevu,waite wataalamu watazame namna bora ya kudhibiti unyevu kwenye eneo lako(nyumba yako)
Kama kuna mabomba yanayovuja,zingatia kuyaziba
Kama bati lako linavuja,zingatia kiuziba


Zipo njia nyingi za kuondoa fangasi kwenye nyumba za asili na za kutumia kemikali. Ni muhimu kuanza na njia za asili kwanza kabla ya kutumia kemikali kuondoa tatizo.Njia hizi hutofautiana kulingana na ukubwa wa tatizo na pia kulingana na sehemu iliyoathiriwa.
·         Kwenye kuta zenye rangi ni muhimu kuondoa kabisa tabaka la rangi lililoathiriwa. Hakikisha unakwangua rangi yote iliyoathiriwa na kuiondoa.
·         Kisha chukua siki nyeupe, robo kikombe ,changanya kwenye maji moto sana lita 2 pamoja na borax vijiko viwili . Koroga vyema mchanganyiko wako. Kisha safisha ukuta wako sehemu iliyoathiriwa na fangasi.Futa kwa kitambaa kama ni ukuta wenye rangi.Fangasi itaondoka.
·         Kwa sehemu ambazo fangasi imeathiri sana tumia dawa ya kuoindoa fangasi(Bleach Based mold remover)
Muhimu kuzingatia ni kwamba njia hii huondoa fangasi iliyopo lakini si kuzuia mazalia mapya hivyo ni muhimu sana kuchukua hatua kwanza kudhibiti unyevu kwenye nyumba yako
Mahitaji
-Robo kikombe cha bleach
Lita 2 ya maji moto
Changanya mchanganyiko wako vema kisha nyunyuzia kwenye sehemu iliyoathiriwa na fangasi
Rudia kunyunyuzia baada ya dakika 15.Kaa baada ya siku 2 na kunyunyuzia tena
(Hakikisha ukuta wako ni mkavu
·         Hakikisha unasafisha vema kuta za bafu na vyoo kwa kutumia dawa yenye siki kama iliyooneshwa hapo juu.Fungua madirisha kwa dakika 15 unapooga ama kutumia bafu. Anika taulo kwenye jua unapolitumia kuzuia kuota kwa fangasi
·         Kama kuta za nyumba hasa za ndani zimeathiriwa sana,badili kuta kwa kutumia vifaa(material) isuiyoathiriwa kwa urahisi na fangasi kama vioo,plastic,kuta za aluminiam na vioo
·         Iwapo sakafu imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na unyevu haukomi,ita wataalamu wabadili sakafu huku wakidhibiti unyevu huku wakitumia vifaa visivyoathiriwa kwa urahisi na unyevu kama tiles(marumaru) ama terrazzo.
·         Kwa rangi za kuta tumia rangi zinastahimili unyevu na fangasi(anti moulds paints),pia tumia lipu inayoweza kustahimili unyevu(anti-mould plaster)
·         Tumia rangi msingi(primer) inayozuia unyevu(barrier primer/anti-mould primer)
·         Iwapo unatumia wall paper(karatasi za kubandika ukutani) hakikisha unaondoa kwanza fangasi kwa kutumia njia iliyotajwa ha[po juu kisha acha ikauke na kubandika karatasi yako
·         Usiweke samani kuegemea ukuta ulioathiriwa na fangasi






Je Makala hii imekusaidia?
Wailiana nami Pongu J
0765046644

No comments: