Katika Makala hii tutajadili tatizo
linalozikumba nyumba nyingi kwenye sehemu za unyevu, ambalo ni la kuta,ceiling,
madirisha, sakafu, msingi na hata milango kushambuliwa na fangasi.
dari iliyoathiriwa na fangasi |
SABABU ZA KUOTA FANGASI KWENYE KUTA
Sababu kuu ya kutokea kwa fangasi kwenye kuta ni Unyevunyevu
, kuganda kwa maji na kuvuja kwa maji
toka kwenye mabomba yaliyopasuka ama kupata ufa.
Kuganda kwa maji hutokea pale mvuke unapokutana na hewa/kitu cha baridi kisha kupoozwa na kuwa maji. Kama kuganda kutachukua muda mrefu kwenye kuta,fangasi huanza kukua kwenye kuta
Mabomba ya maji kwenye nyumba yanapopasuka ama kupata ufa,huruhusu maji kutiririka kenye msingi na kuta.Maji haya hulowesha kuta na msingi na kusababisha kuzaliana kwa fangasi.Fangasi huweza kuonekana kwenye sehemu mbalimbali za nyumba yako kama ifuatavyo
Fangasi kwenye Dari
Hutokana na
unyevunyevu kwenye dari unaoweza kusababishwa na kuvuja kwa maji ama
kuganda kwa maji.
Fangasi kwenye Milango na madirisha
Unyevu kwenye madirisha husababisha kutokea kwa
fangasi.
Fangasi kwenye sakafu
Unyevu kqwenye sakafu nhusababisha kukua kwa
fangasi.Sehemu nyingi ambazo maji hayakauki,hupanda kwenye msingi na kuingia
kwenye sakafu.Ni muhimu sana kuhakikisha hatua za awali za kudhibiti unyevu
kuingia kwenye sakafu zinatiliwa mkazo.
Fangasi kwenye kuta
Unyevu unapopanda kwenye kuta husababisha
fangasi kutokua.Kadiri kuta zinzvyoathiriwa na maji(unyevu) ndivyo fangasi
zinavyokuwa.
Kwenye kuta zinye karatasi(wall paper) Na hata
nguo hushambuliwa
Dalili za fangasi kwenye kuta na sehemu
mbalimbali
Zifuatazo ni dalili kuwa ukuta wako ama
nyumba yanko inashambuliwa na fangasi
1.Kubadilika kwa rangi ya kuta kuwa nyeusi
ama kijani
2.Kubanduka kwa rangi ya nyumba na
nkubadilika
3.Unyevu wa muda mrefu kwenye kuta/sakafu
4.Kutokea kwa alama zenye rangi nnyeusi
kwenye kuta/sakafu
5.Kutokea kwa harufu ya uyoga inayoweza
kusababisha mafua ama chafya
Muhimu: Kuzaliana kwa fangasi kwenye
nyumba yako husababisha madhara makubwa ya kiafya kwa wanaoishi kwenye nyumba
na pia hudhoofisha kuta, rangi,sakafu na hata kuifanya nyumba isiwe imara
Fangasi pia hutokea sana kwenye bafu na
vyoo kutokana na unyevu wa mara kwa mara, hivyo ni muhimu sehemu hizi kutiiwa
mkazo zaidi.
madoa meusi ni dalili ya kuota fangasi kwenye ukuta |
UNAWEZAJE KUONDOA FANGASI KWENYE NYUMBA YAKO(KUTA/SAKAFU)
Kabla ya kujadili namna ya kuondoa fangasi
kwenye nyumba yako,ni muhimu kuzingatia hatua ya awali ya kuzuia kabisa kutokea
kwa unyevunyevu ama maji kwenye kuta/sakafu kwa muda mrefu.
Ni muhimu wakati unajenga kwenye sehemu yenye
unyevu unaotoka ardhini kutumia njia za kuzuia unyevu kupanda kwenye kuta ama msingi.Tumia
Damp roofing membrane/course.Ni muhimu kuzingatia maoni ya wataalamu wakati wa
kujenga.
Kama tayari umejenga kwenye sehemu yenye
unyevu,waite wataalamu watazame namna bora ya kudhibiti unyevu kwenye eneo
lako(nyumba yako)
Kama kuna mabomba yanayovuja,zingatia
kuyaziba
Kama bati lako linavuja,zingatia kiuziba
Zipo njia nyingi za kuondoa fangasi kwenye
nyumba za asili na za kutumia kemikali. Ni muhimu kuanza na njia za asili
kwanza kabla ya kutumia kemikali kuondoa tatizo.Njia hizi hutofautiana
kulingana na ukubwa wa tatizo na pia kulingana na sehemu iliyoathiriwa.
·
Kwenye kuta zenye rangi ni muhimu
kuondoa kabisa tabaka la rangi lililoathiriwa. Hakikisha unakwangua rangi yote
iliyoathiriwa na kuiondoa.
·
Kisha chukua siki nyeupe, robo
kikombe ,changanya kwenye maji moto sana lita 2 pamoja na borax vijiko viwili .
Koroga vyema mchanganyiko wako. Kisha safisha ukuta wako sehemu iliyoathiriwa
na fangasi.Futa kwa kitambaa kama ni ukuta wenye rangi.Fangasi itaondoka.
·
Kwa sehemu ambazo fangasi imeathiri
sana tumia dawa ya kuoindoa fangasi(Bleach Based mold remover)
Muhimu kuzingatia ni kwamba njia hii
huondoa fangasi iliyopo lakini si kuzuia mazalia mapya hivyo ni muhimu sana
kuchukua hatua kwanza kudhibiti unyevu kwenye nyumba yako
Mahitaji
-Robo kikombe cha bleach
Lita 2 ya maji moto
Changanya mchanganyiko wako vema kisha
nyunyuzia kwenye sehemu iliyoathiriwa na fangasi
Rudia kunyunyuzia baada ya dakika 15.Kaa
baada ya siku 2 na kunyunyuzia tena
(Hakikisha ukuta wako ni mkavu
·
Hakikisha unasafisha vema kuta za
bafu na vyoo kwa kutumia dawa yenye siki kama iliyooneshwa hapo juu.Fungua
madirisha kwa dakika 15 unapooga ama kutumia bafu. Anika taulo kwenye jua
unapolitumia kuzuia kuota kwa fangasi
·
Kama kuta za nyumba hasa za ndani
zimeathiriwa sana,badili kuta kwa kutumia vifaa(material) isuiyoathiriwa kwa
urahisi na fangasi kama vioo,plastic,kuta za aluminiam na vioo
·
Iwapo sakafu imeathiriwa kwa kiasi
kikubwa na unyevu haukomi,ita wataalamu wabadili sakafu huku wakidhibiti unyevu
huku wakitumia vifaa visivyoathiriwa kwa urahisi na unyevu kama tiles(marumaru)
ama terrazzo.
·
Kwa rangi za kuta tumia rangi
zinastahimili unyevu na fangasi(anti moulds paints),pia tumia lipu inayoweza
kustahimili unyevu(anti-mould plaster)
·
Tumia rangi msingi(primer) inayozuia
unyevu(barrier primer/anti-mould primer)
·
Iwapo unatumia wall paper(karatasi za
kubandika ukutani) hakikisha unaondoa kwanza fangasi kwa kutumia njia
iliyotajwa ha[po juu kisha acha ikauke na kubandika karatasi yako
·
Usiweke samani kuegemea ukuta
ulioathiriwa na fangasi
Je Makala hii imekusaidia?
Wailiana nami Pongu J
0765046644